Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nimeamrishwa kupigana vita na watu mpaka washuhudie ya kwamba ´hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah`, wasimamishe swalah na watoe zakaah. Wakiyafanya hayo basi imesalimika kwangu damu na mali yao isipokuwa kwa haki yake na hesabu yao iko kwa Allaah (Ta´ala).” [1]
Nini maana ya kwa haki yake?
Jibu: Haki yake ni nguzo za Uislamu. Akikanusha kitu katika nguzo za Uislamu basi anapigwa vita. Ndio maana Abu Bakr as-Swiyddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) aliwapiga vita wenye kukataa kutoa zakaah na akasema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”… isipokuwa kwa haki yake.”
na kwamba zakaah ni katika haki yake. Kwa maana nyingine ni katika haki ya shahaadah.
[1] al-Bukhaariy (25) na Muslim (22).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ad-Durr an-Nadhwiyd (01)
- Imechapishwa: 06/03/2025
Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nimeamrishwa kupigana vita na watu mpaka washuhudie ya kwamba ´hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah`, wasimamishe swalah na watoe zakaah. Wakiyafanya hayo basi imesalimika kwangu damu na mali yao isipokuwa kwa haki yake na hesabu yao iko kwa Allaah (Ta´ala).” [1]
Nini maana ya kwa haki yake?
Jibu: Haki yake ni nguzo za Uislamu. Akikanusha kitu katika nguzo za Uislamu basi anapigwa vita. Ndio maana Abu Bakr as-Swiyddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) aliwapiga vita wenye kukataa kutoa zakaah na akasema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”… isipokuwa kwa haki yake.”
na kwamba zakaah ni katika haki yake. Kwa maana nyingine ni katika haki ya shahaadah.
[1] al-Bukhaariy (25) na Muslim (22).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ad-Durr an-Nadhwiyd (01)
Imechapishwa: 06/03/2025
https://firqatunnajia.com/maana-ya-haki-ya-shahaadah/