Swali: Baadhi ya maamuma wanachukulia vibaya na kusomwa Suurah ”as-Sajdah” na Suurah ”al-Insaan” katika Fajr ya siku ya ijumaa. Imamu anatakiwa kuchukua msimamo gani kwa kuzingatia ya kwamba baadhi wanavutiwa na hilo na wengine hawavutiwi?
Jibu: Katika Fajr hili ni Sunnah. Kusoma Suurah ”as-Sajdah” na kusoma Suurah ”al-Insaan” ni Sunnah aliyoifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imethibiti katika hilo Hadiyth Swahiyh. Hivyo ni Sunnah imamu kusoma katika swalah ya Fajr Suurah as-Sajdah katika Rak´ah ya kwanza na Suurah ”al-Insaan” katika Rak´ah ya pili. Ni Sunnah. Anayechukizwa na hilo ima ni mjinga au ni dhaifu wa imani. Kufufua Sunnah kunahitajika. Kwa hiyo imamu asiwajali wao; atendee kazi Sunnah wala asimjali anayechukizwa na hilo. Apatilize swalah, aiswali kwa utulivu, kutofanya haraka na kusoma yale yaliyosuniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndani yake. Yote haya yanahitajika, hata kama baadhi ya watu wanachukizwa, basi asiache Sunnah kwa ajili ya baadhi ya watu. Apatilize Sunnah na aiharakie katika swalah na mengineyo, hata kama baadhi ya watu wanachukizwa na hilo, kama kusoma Suurah ”as-Sajdah” na Suurah ”al-Insaan”. Haya ni katika Sunnah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1597/السور-التي-يسن-قراءتها-في-صلاة-الفجر-يوم-الجمعة
- Imechapishwa: 27/06/2026
Swali: Baadhi ya maamuma wanachukulia vibaya na kusomwa Suurah ”as-Sajdah” na Suurah ”al-Insaan” katika Fajr ya siku ya ijumaa. Imamu anatakiwa kuchukua msimamo gani kwa kuzingatia ya kwamba baadhi wanavutiwa na hilo na wengine hawavutiwi?
Jibu: Katika Fajr hili ni Sunnah. Kusoma Suurah ”as-Sajdah” na kusoma Suurah ”al-Insaan” ni Sunnah aliyoifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imethibiti katika hilo Hadiyth Swahiyh. Hivyo ni Sunnah imamu kusoma katika swalah ya Fajr Suurah as-Sajdah katika Rak´ah ya kwanza na Suurah ”al-Insaan” katika Rak´ah ya pili. Ni Sunnah. Anayechukizwa na hilo ima ni mjinga au ni dhaifu wa imani. Kufufua Sunnah kunahitajika. Kwa hiyo imamu asiwajali wao; atendee kazi Sunnah wala asimjali anayechukizwa na hilo. Apatilize swalah, aiswali kwa utulivu, kutofanya haraka na kusoma yale yaliyosuniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndani yake. Yote haya yanahitajika, hata kama baadhi ya watu wanachukizwa, basi asiache Sunnah kwa ajili ya baadhi ya watu. Apatilize Sunnah na aiharakie katika swalah na mengineyo, hata kama baadhi ya watu wanachukizwa na hilo, kama kusoma Suurah ”as-Sajdah” na Suurah ”al-Insaan”. Haya ni katika Sunnah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1597/السور-التي-يسن-قراءتها-في-صلاة-الفجر-يوم-الجمعة
Imechapishwa: 27/06/2026
https://firqatunnajia.com/maamuma-wanachukia-imamu-kusoma-as-sajdah-na-al-insaan-katika-fajr-siku-ya-ijumaa/