Swali: Ikiwa swalah imekimiwa na katikati ya swalah nikasahau kusoma al-Faatihah katika Rak´ah moja au mbili huku nikiwa maamuma, je, swalah yangu ni sahihi au la? Je ni lazima nisome Faatihah? Nifanye nini katika hali hii?
Jibu: Ikiwa maamuma atasahau kusoma al-Faatihah, hajui kwamba ni wajibu juu yake au atamkuta imamu akiwa katika Rukuu´, basi katika hali hizi Rak´ah yake inatosha na swalah yake ni sahihi. Halazimiki kuilipa Rak´ah hiyo kwa sababu ana udhuru wa ujinga, kusahau na kutomuwahi imamu katika kisimamo cha kusoma. Haya ndio maoni ya wanazuoni wengi. Hii ni kwa sababu al-Bukhaariy amepokea katika ”as-Swahiyh” yake kutoka kwa Abu Bakrah ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba alimkuta Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika baadhi ya swalah akiwa katika Rukuu´, basi akarukuu nje ya safu kisha akaingia katika safu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
“Allaah akuzidishie pupa, lakini usirudie tena.”[1]
Hakuamrishwa kuilipa Rak´ah hiyo, bali alimkataza kurudia kurukuu nje ya safu.
[1] al-Bukhaariy (783).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/143)
- Imechapishwa: 06/03/2026
Swali: Ikiwa swalah imekimiwa na katikati ya swalah nikasahau kusoma al-Faatihah katika Rak´ah moja au mbili huku nikiwa maamuma, je, swalah yangu ni sahihi au la? Je ni lazima nisome Faatihah? Nifanye nini katika hali hii?
Jibu: Ikiwa maamuma atasahau kusoma al-Faatihah, hajui kwamba ni wajibu juu yake au atamkuta imamu akiwa katika Rukuu´, basi katika hali hizi Rak´ah yake inatosha na swalah yake ni sahihi. Halazimiki kuilipa Rak´ah hiyo kwa sababu ana udhuru wa ujinga, kusahau na kutomuwahi imamu katika kisimamo cha kusoma. Haya ndio maoni ya wanazuoni wengi. Hii ni kwa sababu al-Bukhaariy amepokea katika ”as-Swahiyh” yake kutoka kwa Abu Bakrah ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba alimkuta Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika baadhi ya swalah akiwa katika Rukuu´, basi akarukuu nje ya safu kisha akaingia katika safu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
“Allaah akuzidishie pupa, lakini usirudie tena.”[1]
Hakuamrishwa kuilipa Rak´ah hiyo, bali alimkataza kurudia kurukuu nje ya safu.
[1] al-Bukhaariy (783).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/143)
Imechapishwa: 06/03/2026
https://firqatunnajia.com/maamuma-amesahau-kusoma-al-faatihah-nyuma-ya-imamu/