Maamuma amesahau kusoma al-Faatihah katika swalah ya kusoma kimyakimya

Swali: Niliswali nyuma ya imamu swalah ya ´Aswr na nikasahau kusoma al-Faatihah katika Rak´ah ya kwanza. Je, imamu ananibebea nguzo hii?

Jibu: Ikiwa maamuma amesahau al-Faatihah au alikuwa hajui, basi imamu anambebea. Kama ilivyokuja katika Hadiyth ya Abu Bakrah ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh). Alikuja wakati imamu yuko katika Rukuu´, akarukuu kabla hajafika katika safu kisha akaingia katika safu. Akamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alimwambia:

“Allaah akuzidishie pupa, lakini usirudie tena.”[1]

Hakumuamrisha kulipa Rak´ah ile, kwa sababu hakuhudhuria kisimamo chake.

[1] al-Bukhaariy (783).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/157)
  • Imechapishwa: 07/03/2026