Laana ya Allaah iko juu ya watetezi wa Ahl-ul-Bid´ah na magaidi

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Laana ya Allaah iwe juu ya yule ambaye anamlinda mzushi.”[1]

Je, inahusu mwenye kuwanyamazia na kuwatetea watu wa Bid´ah?

Jibu: Bila ya shaka. Mzushi ni yule mwenye kuzua katika dini ya Allaah mambo yasiyokuwemo. Kadhalika inahusu mtu mwenye kuzua katika mambo ya amani na kuyatikisa.

[1] Muslim (1978).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (32) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20%20-%203-11-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017