Kwanini wanazuoni wote wasikubaliene juu ya ufahamu mmoja?

Swali: Kwa nini wanazuoni wa ummah leo hawakusanyiki na wakawatolea ummah Fiqh moja?

Jibu: Kuwakusanya watu wote si jambo linalowezekana, ni jambo gumu lisilowezekana. Fiqh na dalili zake zinajulikana, vitabu vyao vipo. Mwanafunzi ana vitabu vyake viko mbele yake. Mtu mwenye elimu anaweza kuchukua kutoka ndani ya vitabu vya Hadiyth na vitabu vya wanazuoni yale ambayo atalingania kwayo kwa Allaah na kuwaongoza kwayo ummah. Msingi wa yote hayo ni Kitabu cha Allaah Kitukufu na Sunnah za Mtume Wake mwaminifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31015/لماذا-لا-تجتمع-الامة-على-فقه-موحد
  • Imechapishwa: 21/09/2025