Kuweka mguu juu ya mwingine na kuelekeza miguu Qiblah

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kuelekeza miguu yake upande wa Qiblah?

Jibu: Hakuna tatizo kwake kunyoosha miguu yake kuelekea Qiblah au kujilaza, kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijilaza msikitini. Isipokuwa ikiwa mbele yake kuna msahafu, basi inachukiza kwake kunyoosha mguu wake kuelekea msahafu. Ama ikiwa mbele yake hakuna msahafu, basi hakuna tatizo. Vivyo hivyo ikiwa mbele yake kuna mtu, basi kwa upande wa adabu haifai kufanya hivyo. Ama ikiwa hakuna mtu mbele yake, basi hakuna tatizo kwake kunyoosha miguu yake na pia kupumzika msikitini, kwa sababu imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amelala chali msikitini huku ameweka mguu wake mmoja juu ya mwingine.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 30/09/2026