Swali: Je, Jahmiyyah na Mu´tazilah ni makafiri?

Jibu: Kuna tofauti ya maoni kuhusu hilo. Kuhusu Jahmiyyah wanaokanusha majina na sifa za Allaah, wako wanazuoni ambao wamewakufurisha, wengine wamewatiwa katika Bid´ah na baadhi ya wengine wamewakufurisha wale waliochupa mipaka katika wao. ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba wanazuoni 500 wamewakufurisha Jahmiyyah: Kwa hiyo wengi katika Salaf wamewakufurisha. Miongoni mwa hayo ni maneno yake ´Abdullaah bin al-Mubaarak:

“Kwa hakika sisi tunasimulia maneno ya mayahudi na manaswara, lakini hatusimilii maneno ya Jahmiyyah.”

Hii ni kwa sababu wanapokanusha majina na sifa za Allaah, maana yake ni kwamba hawakuthibitisha kuwepo kwa Allaah. Kwa kuwa hakuna kitu isipokuwa kina sifa na majina. Kitu kisichokuwa na majina wala sifa hakina kuwepo.

Kuhusu Mu´tazilah, wanazuoni wengi wanaona kuwa ni watu wa Bid´ah. Baadhi ya wanazuoni wamewahukumu kuwa ni makafiri.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 30/09/2026