´Abdullaah bin Haraam alizungumzishwa na Allaah

Swali: Je, Allaah alimzungumzisha ´Abdullaah bin Haraam? Je, alimuona Allaah?

Jibu: Allaah alimsemesha kutoka nyuma ya pazia bila ya kuwepo mpatanishi, kama alivyomsemesha Muusa bila ya mpatanishi. Jibriyl alipokuwa akishuka na wahy kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi Jibriyl alikuwa mpatanishi. Allaah alimsemesha Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa kupandishwa mbinguni bila ya Jibriyl kuwa mpatanishi.

Ama kuhusu kumuona Allaah, hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

”Hakika hamtamuona Mola wenu mpaka mfe.”

Kwa hivyo kumuona Allaah hakukuthibiti kwa ´Abdullaah bin Haraam. Kumuona Allaah kutakuwa siku ya Qiyaamah.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 30/09/2026