Swali: Je, inasihi Twawaaf ya mtu ambaye hakuinamia Jiwe Jeusi kwa kulishika ilihali alikuwa ana uwezo wa kufanya hivyo na hakuna mashaka yanayomzuia na akatosheka kwa kulionyesha kwa ishara?
Jibu: Kulishika Jiwe Jeusi, kulibusu na kulionyesha kwa ishara ni Sunnah. Lililo la lazima ni kufanya Twawaaf. Ikiwa masharti ya Twawaaf yametimia na akafanya kuizunguka Nyumba mara saba, kutoka kwenye Jiwe Jeusi mpaka kwenye Jiwe Jeusi, basi ametekeleza lililo juu yake, hata ikiwa hakulionyesha kwa ishara wala hakulishika. Kwa sababu yote hayo ni katika Sunnah. Ikiwa kwenye Jiwe Jeusi kuna manukato, basi mtu aliye ndani ya Ihraam asiliguze.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
- Imechapishwa: 30/09/2026
Swali: Je, inasihi Twawaaf ya mtu ambaye hakuinamia Jiwe Jeusi kwa kulishika ilihali alikuwa ana uwezo wa kufanya hivyo na hakuna mashaka yanayomzuia na akatosheka kwa kulionyesha kwa ishara?
Jibu: Kulishika Jiwe Jeusi, kulibusu na kulionyesha kwa ishara ni Sunnah. Lililo la lazima ni kufanya Twawaaf. Ikiwa masharti ya Twawaaf yametimia na akafanya kuizunguka Nyumba mara saba, kutoka kwenye Jiwe Jeusi mpaka kwenye Jiwe Jeusi, basi ametekeleza lililo juu yake, hata ikiwa hakulionyesha kwa ishara wala hakulishika. Kwa sababu yote hayo ni katika Sunnah. Ikiwa kwenye Jiwe Jeusi kuna manukato, basi mtu aliye ndani ya Ihraam asiliguze.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/inasihi-twawaaf-ya-asiyegusa-jiwe-jeusi/