Swali: Ni halali kwa waislamu kuwasaidia makafiri juu ya kumg´oa kiongozi ambaye amedhihirisha kufuru ya wazi na wanachuoni wamemhukumu kwamba ni kafiri? Kama hayo ni halali ni vipi vidhibiti na masharti yake?
Jibu: Makafiri watamg´oa na wamweke badala yake mwenzao. Mkiwasaidia watamg´oa kweli na wamweke mwezao. Faida iko wapi? Zingatieni! Waislamu wakiwa na nguvu na kumg´oa kiongozi kafiri, watamg´oa. Ama wakiwa hawana nguvu basi wanatakiwa kufanya subira na wasiziweke nafsi zao katika maangamivu na khatari. Ama kusema wawasaidie makafiri kumg´oa hapana. Makafiri wanafurahishwa na hili na wanamweka badala yake mwenzao. Katika hali hiyo sisi tutakuwa tumemwondosha kafiri na tumemlata kafiri mwingine.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (09) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/09.mp3
- Imechapishwa: 30/03/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)