Swali: Nimeweka kiasi cha fedha katika kampuni ya dhahabu kwa ajili ya kuuza na kununua kwa kutumia fedha hiyo na kampuni inapokea 1% ya faida. Kampuni haitoi dhamana ya faida wala khasara.
Jibu: Ukifanya makubaliano na kampuni kuwa itafanya biashara kwa dhahabu yako au fedha zako – ni mamoja iwe ni dhahabu, fedha taslimu au noti – kisha mkakubaliana kuwa kampuni itapata 1% ya faida na yaliyobaki yakawa yako, basi hakuna tatizo. Hiyo 1% ni sehemu ndogo sana ya faida na inakubalika. Kwa mfano ukiipa kampuni shilingi 1000, ikafanya biashara na ikapata faida ya 100, basi kampuni inapewa 1% ya hiyo faida na hilo halina tatizo. Lakini hairuhusiwi kampuni kuchukua asilimia hiyo kutoka kwenye mtaji wala kuahidi kuwa itakupa faida ya kudumu au kudhamini kuwa faida lazima itapatikana. Hilo halijuzu. Hukumu ya uhalali ipo pale tu ambapo malipo yao ni sehemu inayoeleweka ya faida – ni mamoja iwe 1%, 5% au 10% – muda wa kuwa iwe ni sehemu inayojulikana na inayotokana na faida halisi, si kutoka kwenye mtaji.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1122/حكم-ايداع-الاموال-بشركة-مقابل-نسبة-من-الارباح
- Imechapishwa: 30/01/2026
Swali: Nimeweka kiasi cha fedha katika kampuni ya dhahabu kwa ajili ya kuuza na kununua kwa kutumia fedha hiyo na kampuni inapokea 1% ya faida. Kampuni haitoi dhamana ya faida wala khasara.
Jibu: Ukifanya makubaliano na kampuni kuwa itafanya biashara kwa dhahabu yako au fedha zako – ni mamoja iwe ni dhahabu, fedha taslimu au noti – kisha mkakubaliana kuwa kampuni itapata 1% ya faida na yaliyobaki yakawa yako, basi hakuna tatizo. Hiyo 1% ni sehemu ndogo sana ya faida na inakubalika. Kwa mfano ukiipa kampuni shilingi 1000, ikafanya biashara na ikapata faida ya 100, basi kampuni inapewa 1% ya hiyo faida na hilo halina tatizo. Lakini hairuhusiwi kampuni kuchukua asilimia hiyo kutoka kwenye mtaji wala kuahidi kuwa itakupa faida ya kudumu au kudhamini kuwa faida lazima itapatikana. Hilo halijuzu. Hukumu ya uhalali ipo pale tu ambapo malipo yao ni sehemu inayoeleweka ya faida – ni mamoja iwe 1%, 5% au 10% – muda wa kuwa iwe ni sehemu inayojulikana na inayotokana na faida halisi, si kutoka kwenye mtaji.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1122/حكم-ايداع-الاموال-بشركة-مقابل-نسبة-من-الارباح
Imechapishwa: 30/01/2026
https://firqatunnajia.com/kuwapa-kampuni-pesa-wafanye-biashara-na-kupokea-1-ya-faida/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket