Kuvaa pete haikupendezeshwa kwa mujibu wa Shari’ah

Mwanaume kuvaa pete sio katika mambo yaliyopendekezwa. Ni katika mambo ambayo yanafanywa pale ambapo kuna haja ya kufanya hivo. Kama hakuna haja usifanye hivo. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa havai pete. Lakini alipoambiwa kuwa wafalme na marasi anaowaandikia hawakubali barua mpaka iwe imepigwa muhuri, ndipo akatafuta iliyokuwa imeandikwa “Muhammad ni Mtume wa Allaah” ili anapomaliza kuandika barua apige muhuri kwa pete hii.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/445)
  • Imechapishwa: 19/08/2025