Kutupa kucha baada ya kuzikata

Swali: Je, ni sahihi kwamba mtu anayezitupa kucha zake baada ya kuzikata anafanya jambo la haramu? Je, ni kweli kwamba Siku ya Qiyaamah kucha hizo zitachukuliwa kwa kingo za macho?

Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kukata kucha, kwa sababu kuondolewa kwake ni miongoni mwa mambo ya kimaumbile. Hakuna tatizo kuzitupa. Ama yaliyosemwa kwamba kuzitupa ni haramu na kwamba zitachukuliwa kwa kingo za macho siku ya Qiyaamah, si sahihi. Hatujui msingi wowote wa jambo hilo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/174)
  • Imechapishwa: 29/10/2026