Kufupisha nywele kwa sababu ya ugumu wa kuziosha kila mara

Swali 2922: Ni ipi hukumu ya mwanamke kufupisha nywele zake kwa sababu ya dharurah? Kwa mfano nchini Uingereza wanawake wanaona kwamba kuosha nywele nyingi ni vigumu kwao katika hali ya hewa ya baridi na hivyo huzifupisha?

Jibu: Ikiwa hali ni kama ilivyoelezwa, basi inajuzu kwao kufupisha nywele zao kwa kiwango kinachohitajika tu. Ama kuzifupisha kwa lengo la kujifananisha na wanawake makafiri, haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu fulani, basi yeye ni miongoni mwao.”

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/182)
  • Imechapishwa: 29/10/2026