Swali: Kuna mtu ameacha kuswali na kufunga kisha baadaye akatubia kwa Allaah. Ni kipi kinachomlazimu hivi sasa?
Jibu: Wanazuoni wamekinzana kuhusu mtu ambaye ameacha ´ibaadah zilizopangiwa muda maalum mpaka ukamalizika wakati wake pasi na udhuru. Wako waliosema kwamba ni wajibu kwake kuzilipa, wengine wakasema kuwa sio lazima kuzilipa. Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa ambaye anaacha swalah, au kufunga Ramadhaan, kwa makusudi na bila ya udhuru, basi analazimika kuilipa ´ibaadah hiyo. Kwa sababu Allaah amemuwajibishia msafiri na mgonjwa kuzilipa zile siku ambazo hawakufunga. Ikiwa Allaah amemuwajibishia kulipa ambaye yuko na udhuru basi asiyekuwa yeye ana haki zaidi ya kuzilipa. Imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]
Kwa hivyo amemuwajibishia kukidhi na ambaye amesahau na ambaye amepitiwa na usingizi mpaka ukatoka wakati wake. Kwa msemo mwingine wamesema ikiwa imewajibishwa kulipa swalah kwa ambaye yuko na udhuru basi asingekuwa na udhuru ana haki zaidi.
Maoni ya pili yanayosema kuwa ambaye anaacha ´ibaadah iliyopangiwa muda wake kwa makusudi pasi na udhuru, basi sio lazima kwake kuilipa. Kwa sababu ´ibaadah zilizopangiwa muda maalum zinapaswa kufanywa ndani ya kipindi chake maalum kilichopangwa. Akiitoa nje ya muda wake ima kwa kuitanguliza au kwa kuichelewesha haikubaliwi. Kama ambavo mtu akiswali faradhi kabla ya wakati basi swalah yake haikubaliwi. Hukumu ni hiyohiyo ikiwa atafunga kabla ya Ramadhaan basi swawm yake haitokubaliwa. Basi vivyo hivyo endapo atachelewesha swalah kwa wakati wake bila ya udhuru haitokubaliwa kutoka kwake. Kadhalika iwapo atachelewesha swawm ya Ramadhaan pasi na udhuru basi haitokubaliwa kutoka kwake. Haya ndio maoni yenye nguvu. Hilo ni kwa sababu mtu akiitoa ´ibaadah nje ya wakati wake na akaifanya baadaye, atakuwa amefanya kitendo kisichoafikiana na amri ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote atakayefanya kitendo kisichokuwa ndani yake amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[2]
Ikishakuwa kitendo chake ni chenye kurudishwa basi kule kumkalifisha kuikidhi hakuna faida yoyote. Badala yake muulizaji anapaswa kutubia kwa Allaah tawbah ya kweli na ajiongeze matendo mema. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba tawbah ni yenye kufuta yale yaliyotangulia.
[1] al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).
[2] Muslim (1718).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/90-91)
- Imechapishwa: 03/03/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/90-91)
Imechapishwa: 03/03/2026
https://firqatunnajia.com/kutubia-juu-ya-swalah-na-swawm-iliyompita-mtu/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket