Swali: Kuna mtu mmoja amenukuu kutoka kwenu ya kwamba inajuzu kwa anayefanya hajj kutoka Muzdalifah usiku bila udhuru wala sababu. Je, hili ni sahihi?
Jibu: Wanazuoni wameeleza wazi kuwa kutoka iwe katika sehemu ya mwisho ya usiku baada ya nusu ya usiku. Lakini Sunnah ni kwamba asitoke isipokuwa ikiwa yeye ni miongoni mwa wanyonge. Ikiwa ni miongoni mwa wanyonge, kama wanawake, watoto, wazee na wagonjwa, basi Sunnah kwake ni kutoka kabla ya watu, katika mwisho wa usiku. Ama wenye afya njema na wenye nguvu, Sunnah kwao ni kubaki mpaka watoke baada ya alfajiri, baada ya kupambazuka. Haifai kwake kutoka kabla ya hapo na haijuzu. Sahihi ni kuwa haifai kwake kutoka, wala asiye na afya njema, kabla ya nusu ya usiku. Bali iwe ni katika mwisho wa usiku. Lakini mwenye afya njema inampasa abaki mpaka aswali Fajr, kisha atoke pamoja na watu kabla ya kupambazuka. Ama wagonjwa, wazee, wanawake na watoto, basi wao wanatoka katika mwisho wa usiku, katika nusu ya pili ya usiku, na ndugu zao walioko pamoja nao huondoka nao vilevile.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30083/حكم-الدفع-من-مزدلفة-ليلا-بدون-علة-او-عذر
- Imechapishwa: 06/09/2025
Swali: Kuna mtu mmoja amenukuu kutoka kwenu ya kwamba inajuzu kwa anayefanya hajj kutoka Muzdalifah usiku bila udhuru wala sababu. Je, hili ni sahihi?
Jibu: Wanazuoni wameeleza wazi kuwa kutoka iwe katika sehemu ya mwisho ya usiku baada ya nusu ya usiku. Lakini Sunnah ni kwamba asitoke isipokuwa ikiwa yeye ni miongoni mwa wanyonge. Ikiwa ni miongoni mwa wanyonge, kama wanawake, watoto, wazee na wagonjwa, basi Sunnah kwake ni kutoka kabla ya watu, katika mwisho wa usiku. Ama wenye afya njema na wenye nguvu, Sunnah kwao ni kubaki mpaka watoke baada ya alfajiri, baada ya kupambazuka. Haifai kwake kutoka kabla ya hapo na haijuzu. Sahihi ni kuwa haifai kwake kutoka, wala asiye na afya njema, kabla ya nusu ya usiku. Bali iwe ni katika mwisho wa usiku. Lakini mwenye afya njema inampasa abaki mpaka aswali Fajr, kisha atoke pamoja na watu kabla ya kupambazuka. Ama wagonjwa, wazee, wanawake na watoto, basi wao wanatoka katika mwisho wa usiku, katika nusu ya pili ya usiku, na ndugu zao walioko pamoja nao huondoka nao vilevile.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30083/حكم-الدفع-من-مزدلفة-ليلا-بدون-علة-او-عذر
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/kutoka-muzdalifah-usiku-bila-ya-sababu-wala-udhuru-wowote/