Swali: Sherehe nyingi za harusi hazikosi picha za haramu na nisipohudhuria wanazingatia kuwa ni kukata kizazi. Je, inajuzu kwangu kuhudhuria kwa kumuiga ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh)…

Jibu: Hii inahusiana na picha kanisani za manaswara. Picha ni haramu. Wanachuoni wamevua katika hizo zile ambazo ni dharurah peke yake. Amesema (Ta´ala):

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

“Ameshapambanua kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura.” (06:119)

Inajuzu kuchukua picha kwa ajili ya dharurah. Mbali na hizo ni haramu. Picha za kumbukumbu, fani ya picha na mfano wa hizo ni haramu. Haijuzu kuchukua picha ya viumbe wenye roho.

Kuhusiana na kuchukua picha miti, mito, majibali na vitu visivyokuwa na roho ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017