Swali: Je, inajuzu kwa mtu kutoa sehemu ya zakaah ya mali yake kuwapa wahitaji kwa sababu ya haja yao kubwa pamoja na kuzingatia kwamba zakaah hiyo bado haijafikisha wakati wake na muda utafika takriban baada ya miezi miwili?

Jibu: Inajuzu kuharakisha zakaah kwa sababu ya haja. Hakuna neno. Bali inajuzu kuiharakisha miaka miwili kabla haja ikipelekea kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliharakisha zakaah ya ami yake al-´Abbaas wakati alipokuwa akiwa ni mwenye haja.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (14) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-03-11-1434.mp3
  • Imechapishwa: 23/06/2019