Kutembelea makaburi ya waja wema na kutafuta baraka kutoka kwao

Swali: Je, ambaye anaswali, anafunga na anahiji lakini anawatembelea mawalii na anatafuta baraka kutoka kwao – mambo hayo yanaharibu matendo yake mema? Je, akifa anakuwa miongoni mwa watu wa Motoni?

Jibu: Kuhusu kuwatembelea mawalii na waislamu ni jambo limesuniwa. Bali inafaa kuyatembelea makaburi ya makafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliruhusiwa kumtembelea mama yake ambaye ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nilikuwa nimewakatazeni kuyatembelea makaburi. Hivyo basi, yatembeleeni.”

Kuhusu kutafuta baraka, akiona kuwa maiti huyu anaathiri pamoja na Allaah au anaathiri badala ya Allaah, basi hiyo ni shirki. Asipoona kuwa ana uwezo wa kuathiri, basi kutafuta baraka kutoka kwake ni ukhurafi usiyofikia kiwango cha shirki.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 27
  • Imechapishwa: 16/02/2025