Kutafuta msikiti wa imamu mwenye sauti nzuri

Swali 143: Je, inafaa kufuatilia sauti nzuri katika misikiti?

Jibu: Inajuzu ikiwa atapata manufaa kama vile unyenyekevu na mfano wake. Baadhi ya wanazuoni wamechukia hilo. Hata hivyo maoni sahihi ni kwamba inajuzu[1].

[1] Hadiyth ya kukataza haijathibitishwa. Nayo ni ile Hadiyth isemayo:

“Aswali mmoja wenu katika msikiti ulio karibu naye na wala asifuate misikiti.”

Imepokewa na Ibn ´Adiyy katika ”al-Kaamil” (6/2450) na al-´Uqayliy katika ”adh-Dhwu´afaa´” (3/432).

Kuhusu yale yaliyopokewa na at-Twabaraaniy (12/370) kupitia kwa Ibn ´Umar ambaye amesimulia:

“Aswali mmoja wenu msikitini mwake na wala asifuatilie misikiti.”,

hakikuhifadhiwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 69
  • Imechapishwa: 27/03/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´