Kuswali kwenye msikiti uliopambwa picha za watu na wanyama

Swali: Baadhi ya misikiti inapambwa marumaru nyeusi na nyeupe kwa ndani. Kwa masikitiko makubwa ni kwamba marumaru hizi zimeletwa kutoka katika nchi za kikafiri na za kishirikina na kwa ajili hiyo zinakuwa na picha zilizofunikwa za watu na wanyama zilizo dhahiri na zilizojificha. Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya misikiti hii na kuweka marumaru hizi kama hizi ndani ya misikiti?

Jibu: Ni haramu kuweka marumaru hizi zinazodhihiri picha. Ni haramu kuweka ndani ya misikiti ya waislamu marumaru yenye picha. Waswaliji wa kitongoji hicho wanalazimika kuwataka kuyaondosha. Isipowezekana, basi wasiswali ndani ya msikiti huu. Bali watafute misikiti mingine. Kwa ajili hiyo ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akikataa kuingia kwenye makanisa, kwa sababu yako na picha.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/349)
  • Imechapishwa: 11/04/2026