Kuswali kwa kuelekea chetezo na hita za umeme

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka chetezo mbele ya waswaliji msikitini?

Jibu: Hapana vibaya na wala hili haliingii katika yale yaliyotajwa na baadhi ya wanazuoni kwamba inachukiza kuswali kwa kuuelekea moto. Wale waliosema kuwa inachukiza kuswali kwa kuuelekea moto wametoa sababu kwamba kitendo hicho kinafanana na ´ibaadah ya waabudia moto. Waabudia moto hawaabudu moto kwa njia hii na kwa ajili hiyo hapana vibaya kuweka chetezo wala pia kuweka hita za umeme mbele ya waswaliji, khaswa ikiwa mbele ya waswaliji peke yao na si mbele ya imamu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/409-410)
  • Imechapishwa: 10/04/2026