211 – Nilimuuliza Shaykh wetu kuhusu Hadiyth ya ‘Utbaan bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh)[1] nambari (1186) kama kunachukuliwa kutoka humo usuniwaji wa kuswali Dhuhaa kwa pamoja?

Jibu: Ndiyo, katika nyumba.

212 – Mtu mwingine akamuuliza kama inafaa kufanya hivo msikitini?

Jibu: Inaweza kutokea kufahamiana makosa, kwa sababu inafanana na swalah ya faradhi.

[1] Nilimuuliza Shaykh wetu Ibn ´Uthaymiyn ´Unayzah kuhusu Hadiyth ya Ibn Umm Maktuum kwamba hakumpa idhini ya kuacha swalah ya mkusanyiko, hata hivyo akampa idhini ´Utbaan? Akajibu: ”Ibn Umm Maktuum anasikia adhaana, lakini hali siyo hivo kwa ´Utbaan.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 90
  • Imechapishwa: 01/05/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´