Mtu akisema kwamba iwapo Allaah yuko juu ya ´Arshi basi hiyo inapelekea kwamba ima ni mkubwa zaidi kuliko ´Arshi, mdogo kuliko ´Arshi au analingana na ´Arshi na kwamba ni jambo lisilowezekana kabisakabisa, basi atambue kuwa hakufahamu kuhusu Allaah kuwa juu ya ´Arshi isipokuwa vile anavyofahamu kuhusu miili iliyoumbwa. Malazimsiho haya yametokana na uelewa huu.

Kuhusiana na kustawa ambako kunalingana na utukufu wa Allaah na ni maalum Kwake, basi hakupelekei katika malazimisho yoyote ya batili. Anayesema hivo anakumbushia yule mwenye kusema kwamba ikiwa viumbe wana Muumba, basi ima awe jauhari au aradhi na yote mawili hayawezekani katukatu. Kwa sababu hakuna kilichopo isipokuwa kwa mambo haya. Aidha anasema kuwa ikiwa Allaah amelingana juu ya ´Arshi, anafanana na namna mtu anavyolingana juu ya kiti au ndani ya meli – hakuna kulingana kunakotambulika zaidi ya huku. Mtu mwenye kufikiria namna hii hafahamu jengine zaidi ya kiumbe anavyolingana.

Haki ni yale waliyowafikiana juu yake Ummah wa kati na kati; ya kwamba Allaah amelingana juu ya ´Arshi vile inavyolingana na utukufu Wake. Kama ambavyo anasifiwa kwamba ni mjuzi wa kila kitu, ni Mwenye kuona na ni muweza wa kila kitu kwa njia isiyofanana na sifa za viumbe, vivyo hivyo amelingana juu ya ´Arshi kwa njia isiyofanana na kulingana kwa viumbe – Ametakasika Allaah kutokamana na hilo.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (5/27-28)
  • Imechapishwa: 13/04/2019