Swali: Je, Adhkaar za wakati wa kulala na mfano wake zinaingia katika makatazo kama mfano wa kusoma Qur-aan?

Jibu: Hapana ikiwa makusudio sio kisomo [cha Qur-aan] bali ni kusoma Adhkaar tu. Kusoma baadhi ya Aayah hakuna neno midhali mtu hakufanya hivo kwa malengo ya kusoma bali amesoma kwa lengo la Adhkaar kama du´aa isemayo:

ربنا لا تزغ قلوبنا بعد إذ هديتنا

“Ee Mola wetu! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kuzihidi.”

Hii haizingatiwi ni kusoma Qur-aan.

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimtaja Allaah katika hali zake zote.

Jibu: Adhkaar sio sawa na kisomo. Adhkaar imeenea zaidi kuliko kisomo.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://mdkhly.com/1418
  • Imechapishwa: 25/11/2017