Kusikiliza nyimbo na muziki ni katika dhambi kubwa?

Swali: Je, kusikiliza nyimbo na kuzirudia ni katika madhambi makubwa?

Jibu: Ikiwa ni nyimbo zinazochochea nafsi, kama miziki ya shaytwaan, wanazuoni wametaja kwamba ni katika ufasiki. Kwa maana kusikiliza nyimbo na kujistarehesha nazo. Na si jambo lililo mbali kuwa ni katika madhambi makubwa ikiwa mwenye kufanya maasi anaendelea kushikamana na nyimbo na amekuwa mzoefu nazo.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 10/10/2026