Du´aa kwa ajili ya kuingia mwaka mpya wa Kiislamu

Swali: Ni ipi hukumu ya kusema mwanzoni mwa mwaka mpya wa Kiislamu?

كل عام وأنتم بخير

“Uwe na mwaka mpya wenye furaha.”?

Je, kuna neno la maelekezo katika suala hili kuhusu elimu, matendo na ulingano?

Jibu: Sijui msingi wowote wa hilo. Lakini huenda likawa katika mlango wa du´aa ya jumla, kwa maana kwamba muislamu kumuombea ndugu yake. Asili ya du´aa ni jambo limewekwa katika Shari´ah.

Inampasa kila muislamu kutumia fursa ya umri, kuzidisha matendo mema, kutekeleza yale aliyolazimishwa na kuacha yale Allaah aliyoyaharamisha katika kila wakati. Aidha akumbuke kupita kwa miaka, miezi na siku na mwisho wa umri na kwamba miaka inapita mwaka baada ya mwaka. Kadhalika miezi na siku na kwamba yote hayo yanamfikisha mtu kwenye muda wake wa kufa. Kwa hiyo inampasa mtu kukumbuka. Kila anapozidi umri azidi pia katika matendo mema.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 10/10/2026