12- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Yaziyd bin Sinaan ametuhadithia Misri: Abu Bakr al-Hanafiy ametuhadithia: ´Abdul-Hamiyd bin Ja´far ametuhadithia: al-Maqbariy amenihadithia, kutoka kwa ´Awn bin ´Abdillaah bin ´Utbah, kutoka kwa Ibn Mas´uud aliyesema:
“Siku moja wakati tulipokuwa tumeketi msikitini pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja mwanamume kutok katika Banuu Sulaym akiitwa ´Amr bin ´Utbah. Alikuwa amemfuata (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Makkah na hakumuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa mpaka alipofika al-Madiynah. Akaja na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Nifunze kitu unachojua ambacho mimi sikijui na ambacho kitaninufaisha, na wala usirefushe. Ni swalah ipi ya mchana au usiku ambayo ni salama zaidi?” Mwishoni akasema: “Ni swalah ya sunnah ambayo ni bora zaidi?” Akasema: “Wakati kunapoenda theluthi ya usiku (au alisema “nusu ya usiku”). Katika wakati huo hushuka Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall) katika mbingu ya dunia na kusema: “Hakuna mtenda dhambi aniombae msamaha nimghufurie? Hakuna mwombaji ambaye analililia Nimpe maombi yake? Au hakuna mwenye huzuni nimsahilishie?” Mpaka alfajiri inapoingia Mwingi wa huruma hupanda, Aliye mtukufu, Aliye juu kabisa (´Azza wa Jall).”
- Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 100-101
- Imechapishwa: 15/01/2018
12- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Yaziyd bin Sinaan ametuhadithia Misri: Abu Bakr al-Hanafiy ametuhadithia: ´Abdul-Hamiyd bin Ja´far ametuhadithia: al-Maqbariy amenihadithia, kutoka kwa ´Awn bin ´Abdillaah bin ´Utbah, kutoka kwa Ibn Mas´uud aliyesema:
“Siku moja wakati tulipokuwa tumeketi msikitini pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja mwanamume kutok katika Banuu Sulaym akiitwa ´Amr bin ´Utbah. Alikuwa amemfuata (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Makkah na hakumuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa mpaka alipofika al-Madiynah. Akaja na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Nifunze kitu unachojua ambacho mimi sikijui na ambacho kitaninufaisha, na wala usirefushe. Ni swalah ipi ya mchana au usiku ambayo ni salama zaidi?” Mwishoni akasema: “Ni swalah ya sunnah ambayo ni bora zaidi?” Akasema: “Wakati kunapoenda theluthi ya usiku (au alisema “nusu ya usiku”). Katika wakati huo hushuka Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall) katika mbingu ya dunia na kusema: “Hakuna mtenda dhambi aniombae msamaha nimghufurie? Hakuna mwombaji ambaye analililia Nimpe maombi yake? Au hakuna mwenye huzuni nimsahilishie?” Mpaka alfajiri inapoingia Mwingi wa huruma hupanda, Aliye mtukufu, Aliye juu kabisa (´Azza wa Jall).”
Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 100-101
Imechapishwa: 15/01/2018
https://firqatunnajia.com/kushuka-kwa-allaah-kupitia-upokezi-wa-abdullaah-bin-masuud-5/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)