Swali: Ni ipi hukumu ya watu wa mkusanyiko kusalimiana baadhi yao kwa baadhi baada ya swalah khaswa ya Fajr? Nimesikia wengine wakisema ni Bid´ah na wengine wanasema hakuna tatizo ndani yake. Ni yepi maoni sahihi katika hilo?
Jibu: Hatujui ubaya ndani ya hilo. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alimuitikia salamu bedui aliyekuja msikitini akaswali lakini hakukamilisha swalah yake. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
“Rudi ukaswali, kwa sababu hujaswali.”
Kwa hiyo akarudi akaswali, kisha akaja akamsalimia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akamuitikia salamu yake kisha akamwambia:
“Rudi ukaswali, kwa sababu hujaswali… ”[1]
Hadiyth hii imo kwa al-Bukhaariy na Muslim. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumkatalia salamu yake ya pili wala ya tatu, bali alimkubalia na akamjibu salamu yake, hali ya kuwa alikuwa anaswali karibu naye na hakumkosa. Kwa sababu kubadilishana salamu kati ya mkusanyiko wa watu kunaleta kupatana kwa nyoyo na kuthibitisha mapenzi.
[1] al-Bukhaariy (757):
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/316)
- Imechapishwa: 09/03/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya watu wa mkusanyiko kusalimiana baadhi yao kwa baadhi baada ya swalah khaswa ya Fajr? Nimesikia wengine wakisema ni Bid´ah na wengine wanasema hakuna tatizo ndani yake. Ni yepi maoni sahihi katika hilo?
Jibu: Hatujui ubaya ndani ya hilo. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alimuitikia salamu bedui aliyekuja msikitini akaswali lakini hakukamilisha swalah yake. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
“Rudi ukaswali, kwa sababu hujaswali.”
Kwa hiyo akarudi akaswali, kisha akaja akamsalimia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akamuitikia salamu yake kisha akamwambia:
“Rudi ukaswali, kwa sababu hujaswali… ”[1]
Hadiyth hii imo kwa al-Bukhaariy na Muslim. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumkatalia salamu yake ya pili wala ya tatu, bali alimkubalia na akamjibu salamu yake, hali ya kuwa alikuwa anaswali karibu naye na hakumkosa. Kwa sababu kubadilishana salamu kati ya mkusanyiko wa watu kunaleta kupatana kwa nyoyo na kuthibitisha mapenzi.
[1] al-Bukhaariy (757):
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/316)
Imechapishwa: 09/03/2026
https://firqatunnajia.com/kusalimiana-waswaliji-baada-ya-swalah/