Kusafirisha na kutawanya mizigo ya haramu

Swali: Mimi nafanya kazi posta na baadhi ya nyakati napata mizigo ambayo ina kanda za muziki na picha chafu. Je, amana hii ni lazima kuifikisha kwa wenye nayo au niharibuharibu pasi na wahusika wala wenye mizigo yao kujua ?

Jibu: Huu wa pili ndio mfano ambao unatakiwa kutajwa. Mfano wa mambo kama haya kuhayaribu hakuzingatiwi ni usaliti. Bali ni katika amana. Ukijua ndani ya mzigo fulani kuna mambo yaliyoharamishwa na Allaah au mambo yanayoita katika yaliyoharamishwa na Allaah, basi ni lazima kuharibu. Ni lazima kuharibu yale yaliyomo ndani katika kaseti mbaya ambazo zinalingania katika batili na picha chafu zinazoita katika batili. Hakuna haja ya kuwataka idhini wahusika. Ukijua jambo hilo kwa kujionea mwenyewe kwa macho yako basi ni lazima kuharibu. Kufanya hivo ni katika kukemea maovu. Kumfikishia mwenye nayo ni katika usaliti na si katika kutekeleza amana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fatawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4264/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B1%D8%B3%D8%A7%D9%89%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D8%B1%D9%8A%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%8A-%D8%A8%D9%87%D8%A7-%D9%85%D9%86%D9%83%D8%B1%D8%A7%D8%AA
  • Imechapishwa: 27/05/2020