Swali: Ikiwa wakati wa swalah msikitini na mkusanyiko wako katika Rukuu´ – je, inajuzu nirukuu hali ya kuwa mbali na mkusanyiko wala hakuna aliye karibu yangu, kisha baada ya kunyooka nisonge mbele hadi nijiunge na safu pamoja na wengine?
Jibu: Hili lilimtokea Maswahabah fulani (Radhiya Allaahu ´anh), naye ni Abu Bakrah ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh). Alikuja siku moja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa katika Rukuu´, basi akarukuu nje ya safu, kisha akatembea na kujiunga na safu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotoa salamu akauliza kuhusu jambo hilo, kana kwamba alilihisi. Alikuwa akiona walio nyuma yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Miongoni mwa mambo maalum kwake ni kwamba alikuwa anaona walio nyuma yake. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
”Allaah akuzidishie hima, lakini usirudie tena.”
Akamkataza arudie kurukuu nje ya safu. Kwa hiyo hili linajulisha ya kwamba ni wajibu kusubiri mpaka mtu afike safuni. Haifai kurukuu peke yake. Kwa hiyo asubiri mpaka afike safuni na azibe pengo, au afike mwisho wa safu na asimame pamoja na watu. Haifai kwa mtu kuswali peke yake wala kurukuu peke yake. Bali asubiri mpaka awe pamoja na mwingine, azibe pengo katika safu au mwishoni mwa safu aingie humo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29989/هل-يجوز-الركوع-بعيدا-عن-الصف-لادراك-الجماعة
- Imechapishwa: 25/08/2025
Swali: Ikiwa wakati wa swalah msikitini na mkusanyiko wako katika Rukuu´ – je, inajuzu nirukuu hali ya kuwa mbali na mkusanyiko wala hakuna aliye karibu yangu, kisha baada ya kunyooka nisonge mbele hadi nijiunge na safu pamoja na wengine?
Jibu: Hili lilimtokea Maswahabah fulani (Radhiya Allaahu ´anh), naye ni Abu Bakrah ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh). Alikuja siku moja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa katika Rukuu´, basi akarukuu nje ya safu, kisha akatembea na kujiunga na safu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotoa salamu akauliza kuhusu jambo hilo, kana kwamba alilihisi. Alikuwa akiona walio nyuma yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Miongoni mwa mambo maalum kwake ni kwamba alikuwa anaona walio nyuma yake. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
”Allaah akuzidishie hima, lakini usirudie tena.”
Akamkataza arudie kurukuu nje ya safu. Kwa hiyo hili linajulisha ya kwamba ni wajibu kusubiri mpaka mtu afike safuni. Haifai kurukuu peke yake. Kwa hiyo asubiri mpaka afike safuni na azibe pengo, au afike mwisho wa safu na asimame pamoja na watu. Haifai kwa mtu kuswali peke yake wala kurukuu peke yake. Bali asubiri mpaka awe pamoja na mwingine, azibe pengo katika safu au mwishoni mwa safu aingie humo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29989/هل-يجوز-الركوع-بعيدا-عن-الصف-لادراك-الجماعة
Imechapishwa: 25/08/2025
https://firqatunnajia.com/kurukuu-kabla-ya-kufika-kwenye-safu/