Swali: Kuna watu wameswali kuelekea Qiblah kwa kutumia dira – isipokuwa mtu mmoja ambaye ametofautiana na wenziwe. Ni ipi hukumu?
Jibu: Nafikiria kuwa mtu huyu ambaye ametofautiana na ndugu isipokuwa ni kwa sababu anafikiria kuwa yuko katika haki. Kwa ajili hiyo analipwa thawabu juu ya kitendo chake, lakini amekosea katika kitendo chake kwa sababu ametofautiana na kupingana na mkusanyiko wake. Ikibainika itabaini kuwa dira ndio ilikuwa imepatia, basi ameingia katika makosa mawili.
1 – Ameswali kinyume na Qiblah. Hilo linaiathiri swalah yake na pengine hata kuibatilisha ikiwa amepinda sana kutokana na Qiblah.
2 – Ametofautiana na mkusanyiko. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ima mtazinyoosha safu zenu au Allaah atakutofautisheni kati ya nyuso zenu.”[1]
Kwa maana ya kwamba watatofautiana na kutofautiana kwa umoja wao. Ikiwa haya ni juu ya mtu ambaye ametangulia mbele kidogo, vipi kwa ambaye ametofautiana na mkusanyiko na akaelekea upande wa kimakosa? Kwa hivyo ni lazima kwa bwana huyu kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na asipingane na yale yanayofahamishwa na kifaa hiki. Kwa sababu vifaa hivi vimekuwa ni kama hoja imara kutokana na ubobeaji wa elimu na umakini wake. Vinapoonyesha upande fulani, basi mara nyingi huwa usahihi ni hivo. Sioni kuwa inafaa kwa bwana huyu kwenda kinyume na mkusanyiko wake. Tukikadiria kuwa yeye ndiye imamu, basi aelekee upande wa msikiti na si upande wa vile yeye anavyofikiria – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] al-Bukhaariy (717) na Muslim (436).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/418-419)
- Imechapishwa: 13/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/418-419)
Imechapishwa: 13/04/2026
https://firqatunnajia.com/kupuuza-dira-ya-waswaliji-wengine/