Swali: Msichana aliye katika mwanzo wa umri wake ana nyusi zenye manyoya mengi sana kiasi kwamba zinakaribia kuwa mbaya kwa muonekano. Msichana huyu alilazimika kunyoa baadhi ya sehemu zinazotenganisha nyusi mbili na kupunguza yaliyobaki ili muonekano uwe wa kawaida kwa ajili ya mume wake. Wakaamua kumrejea mwenye ujuzi wa mambo kama haya ya Shari´ah ambayo yanawatatiza watu wengi. Je, msichana huyu aendelee na hali hiyo aliyo nayo?

Jibu: Haijuzu kunyoa nyusi wala kuzipunguza, kwa sababu hilo ni (النمص) ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kulifanya au kuomba lifanyiwe. Kwa hiyo ni wajibu kwako kutubu na kuomba msamaha kwa yaliyopita. Aidha ujihadhari na jambo hilo wakati ujao.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/196)
  • Imechapishwa: 31/10/2026