Swali: Baadhi ya ndugu wameenda mbali katika kuchukua kutoka kwenye ndevu na wanasema kwamba hizi ni nyuzi zisizohitajika na ziada na wakidai kwamba hilo ni jambo lililotajwa na baadhi ya wanazuoni.
Jibu: Anapaswa kufundishwa kwamba hilo ni kosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kateni masharubu na ziacheni ndevu. Jitofautisheni na washirikina.”
Ameipokea al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake.
Imekuja katika tamko jengine:
“Kateni masharubu na fugeni ndevu. Jitofautisheni na washirikina.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Imekuja katika tamko la tatu kwa Muslim:
“Punguzeni masharubu na ziacheni ndevu. Jitofautisheni na waabudia moto.”
Kwa hiyo ni wajibu kuziacha ndevu, kuzitukuza na kuziacha zikue bila kufuata ruhusa ya mtu yeyote.
Swali: Vipi ikiwa atatoa hoja kwa kitendo cha baadhi ya Maswahabah?
Jibu: Je, Swahabah amekingwa na kukosea? Aliyekingwa na makosa ni yule anayefikisha kutoka kwa Allaah. Hivyo shikamana na aliyekingwa na makosa na mwache ambaye hakukingwa na makosa, kwani wao mara hukosea na mara hupatia. Mwombee kwa Allaah amsamehe. Ikiwa Ibn ´Umar, Zayd, ´Amr, Ahmad bin Hanbal, ash-Shaafi´iy au mmoja wa waliokuja baadaye au wengineo amekosea, basi mwombee kwa Allaah amsamehe. Shikamana na haki. Usiaache haki kwa ajili ya maneno ya yeyote, si kwa maneno ya as-Swiddiyq, ´Umar, ´Uthmaan, Ibn Hanbal, ash-Shaafi´iy, Zayd wala ´Amr. Haki imo juu ya wote mara inapodhihiri na kubainika, lakini pamoja na kuwaridhia watu wa kheri, kuwarehemu na kuwadhania vizuri.
Swali: Je, kunyoa ndevu ni dhambi kubwa kati ya madhambi makubwa?
Jibu: Ni maasi. Lakini kusema kwamba ni dhambi kubwa, Allaah ndiye anayejua zaidi. Ni miongoni mwa maasi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31628/ما-حكم-الاخذ-من-اللحية-استىناسا-بفعل-صحابي
- Imechapishwa: 11/11/2025
Swali: Baadhi ya ndugu wameenda mbali katika kuchukua kutoka kwenye ndevu na wanasema kwamba hizi ni nyuzi zisizohitajika na ziada na wakidai kwamba hilo ni jambo lililotajwa na baadhi ya wanazuoni.
Jibu: Anapaswa kufundishwa kwamba hilo ni kosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kateni masharubu na ziacheni ndevu. Jitofautisheni na washirikina.”
Ameipokea al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake.
Imekuja katika tamko jengine:
“Kateni masharubu na fugeni ndevu. Jitofautisheni na washirikina.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Imekuja katika tamko la tatu kwa Muslim:
“Punguzeni masharubu na ziacheni ndevu. Jitofautisheni na waabudia moto.”
Kwa hiyo ni wajibu kuziacha ndevu, kuzitukuza na kuziacha zikue bila kufuata ruhusa ya mtu yeyote.
Swali: Vipi ikiwa atatoa hoja kwa kitendo cha baadhi ya Maswahabah?
Jibu: Je, Swahabah amekingwa na kukosea? Aliyekingwa na makosa ni yule anayefikisha kutoka kwa Allaah. Hivyo shikamana na aliyekingwa na makosa na mwache ambaye hakukingwa na makosa, kwani wao mara hukosea na mara hupatia. Mwombee kwa Allaah amsamehe. Ikiwa Ibn ´Umar, Zayd, ´Amr, Ahmad bin Hanbal, ash-Shaafi´iy au mmoja wa waliokuja baadaye au wengineo amekosea, basi mwombee kwa Allaah amsamehe. Shikamana na haki. Usiaache haki kwa ajili ya maneno ya yeyote, si kwa maneno ya as-Swiddiyq, ´Umar, ´Uthmaan, Ibn Hanbal, ash-Shaafi´iy, Zayd wala ´Amr. Haki imo juu ya wote mara inapodhihiri na kubainika, lakini pamoja na kuwaridhia watu wa kheri, kuwarehemu na kuwadhania vizuri.
Swali: Je, kunyoa ndevu ni dhambi kubwa kati ya madhambi makubwa?
Jibu: Ni maasi. Lakini kusema kwamba ni dhambi kubwa, Allaah ndiye anayejua zaidi. Ni miongoni mwa maasi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31628/ما-حكم-الاخذ-من-اللحية-استىناسا-بفعل-صحابي
Imechapishwa: 11/11/2025
https://firqatunnajia.com/kupunguza-ndevu-kwa-kujengea-hoja-ya-swahabah/