Kupuliza hewa kwenye mnyama wakati wa kumchuna

Swali: Katika machinjio ya kusini mwa Riyaadh niliingia na kuwakuta wanapuliza hewa kwenye mnyama aliyechinjwa. Je, upi mtazamo wa Shari´ah kuhusu hilo?

Jibu: Kupuliza hewa hakuna ubaya. Kuacha ni bora zaidi, lakini si haramu. Kuacha kupuliza ni bora. Kuchuna ngozi bila kupuliza hewa ikiwa kuna uwezekano, hiyo ni bora zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1958/حكم-نفخ-الذبيحة
  • Imechapishwa: 30/05/2026