Kupangusa shingo wakati wa kutawadha

Swali: Je, kupangusa shingo katika wudhuu´ si jambo linalopendekezwa kwa sababu ni kufanana na mayahudi kutokana na nilivyosikia?

Jibu: Kupaka shingo si jambo linalopendekezwa wala haikuwekwa katika Shari´ah. Kupaka kunakuwa kwa kichwa na masikio tu, kama ilivyojulisha Qur-aan na Sunnah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/102)
  • Imechapishwa: 19/02/2026