Swali: Je, inasihi nioshe baadhi ya viungo mara tatu na baadhi ya vingine mara mbili?
Jibu: Hapana tatizo kuosha baadhi ya viungo mara mbili, baadhi mara tatu, baadhi mara moja, baadhi mara mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitawadha mara mojamoja, mara mbilimbili, mara tatutatu. Aliwahi kuosha baadhi ya viungo mara mbili na baadhi mara tatu. Hivyo akiosha uso wake mara tatu, kila mkono mara mbili, au akiosha miguu yake mara tatu au mara mbili, hakuna tatizo. Lakini kilicho bora ni mara tatutatu; aoshwe uso mara tatu na mikono mara tatu. Kichwa hupanguswa mara moja tu; hakirudiwi kupangusa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31703/ما-حكم-تفاوت-عدد-غسل-الاعضاء-في-الوضوء
- Imechapishwa: 16/11/2025
Swali: Je, inasihi nioshe baadhi ya viungo mara tatu na baadhi ya vingine mara mbili?
Jibu: Hapana tatizo kuosha baadhi ya viungo mara mbili, baadhi mara tatu, baadhi mara moja, baadhi mara mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitawadha mara mojamoja, mara mbilimbili, mara tatutatu. Aliwahi kuosha baadhi ya viungo mara mbili na baadhi mara tatu. Hivyo akiosha uso wake mara tatu, kila mkono mara mbili, au akiosha miguu yake mara tatu au mara mbili, hakuna tatizo. Lakini kilicho bora ni mara tatutatu; aoshwe uso mara tatu na mikono mara tatu. Kichwa hupanguswa mara moja tu; hakirudiwi kupangusa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31703/ما-حكم-تفاوت-عدد-غسل-الاعضاء-في-الوضوء
Imechapishwa: 16/11/2025
https://firqatunnajia.com/kuosha-viungo-vya-wudhuu-mara-zinazotofautiana/