Swali: Baadhi ya watu hulala wakati wa Khutbah ya ijumaa. Je, tukiwaamsha tutakuwa katika wale waliofanya upuuzi na hivyo hawana swalah ya ijumaa?
Jibu: Inapendekezwa kuwaamsha kwa kitendo, si kwa maneno. Kwa sababu kuzungumza wakati wa Khutbah hakujuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ukimwambia mwenzako ”Nyamaza!” siku ya ijumaa na imamu anakhutubu, basi umefanya upuuzi.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuita huyo kuwa amefanya upuuzi ilihali anamwamrisha mema. Hilo linafahamisha wajibu wa kusikiliza kwa makini na uharamu wa kuzungumza wakati wa Khutbah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/252)
- Imechapishwa: 23/02/2026
Swali: Baadhi ya watu hulala wakati wa Khutbah ya ijumaa. Je, tukiwaamsha tutakuwa katika wale waliofanya upuuzi na hivyo hawana swalah ya ijumaa?
Jibu: Inapendekezwa kuwaamsha kwa kitendo, si kwa maneno. Kwa sababu kuzungumza wakati wa Khutbah hakujuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ukimwambia mwenzako ”Nyamaza!” siku ya ijumaa na imamu anakhutubu, basi umefanya upuuzi.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuita huyo kuwa amefanya upuuzi ilihali anamwamrisha mema. Hilo linafahamisha wajibu wa kusikiliza kwa makini na uharamu wa kuzungumza wakati wa Khutbah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/252)
Imechapishwa: 23/02/2026
https://firqatunnajia.com/kumwamsha-mwenye-kulala-siku-ya-ijumaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket