Swali: Akimuwekea sharti walii wa mwanamke mume asioe mwanamke wapili, na mume akakubali hilo wakati wa ndoa. Je, inasihi sharti hiyi? Na je, akioa mwanamke mwengine ni haki kwake kufarakana naye?

Jibu: Ndiyo, sahihi ni kuwa inasihi kuweka sharti. Kutokana na kauli za wanazuoni. Akimuwekea sharti asioe mwanamke mwengine, sharti ni sahihi. Kwa kuwa ni jambo lina maslahi wakati wa madhara. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waislamu wako kwa masharti yao.”

Akikubali mume kuwa hatooa mwanamke mwengine, ni lazima atekeleze sharti. Ikitokea akaoa, hana neno [mume]. Lakini mwanamke yule ana khiyari ya kufarakana naye [kama anapenda hilo], au kusubiri na kusamehe hilo hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid= 8177
  • Imechapishwa: 10/04/2022