Kumuona binamu ambaye alinyonyeshwa na mama yangu

Swali: Nina binti wa ami yangu nataka kumuoa, lakini yeye alinyonya pamoja na wengi wa ndugu zangu kutoka kwa mama yangu na si kutoka kwa baba yangu. Maziwa yalikuwa ya mume aliyekuwa kabla ya baba yangu, kwani mama yangu alikuwa amepewa talaka naye. Lakini mama yangu hajui alimnyonyesha mara ngapi – mara tatu, mbili au zaidi. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Unyonyeshaji unaosababisha uharamu ni lazima uwe mara zisizopungua tano ndani ya kipindi cha miaka miwili ya kwanza. Hili limethibiti katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba:

”Awali kulikuwa na unyonyeshaji kumi unaoharamisha, kisha ukafutwa na kubaki tano.”

Imekuja katika Hadiyth nyingine ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Sahlah bint Suhayl:

“Mnyonyeshe Saalim mara tano na hivyo atakuwa haramu kwako.”

Hivyo ni lazima kuwe na unyonyeshaji mara zisizopungua tano. Ikiwa mama, ambaye ni mnyonyeshaji, hajui kama alimnyonyesha mara moja, mbili, tatu au zaidi, basi unyonyeshaji huo hauhesabiwi na hauleti uharamu.

Kwa hiyo huyo aliyenyonyeshwa hahesabiwi kuwa ni mtoto wake, si ndugu wa watoto wake wala si mtoto wa mume mwenye maziwa mpaka pale unyonyeshaji utakapofikia mara tano au zaidi na uwe ndani ya miaka miwili ya mwanzo wa mtoto. Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakuna unyonyeshaji isipokuwa ndani ya miaka miwili.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3339/مقدار-الرضاع-الذي-يحصل-به-التحريم
  • Imechapishwa: 03/10/2026