Swali: Ni ipi hukumu ya kuacha kuhukumu kwa Shari´ah ya Allaah? Je, ni jambo linamtoa katika Uislamu? Je, anakuwa ni fasiki, au kafiri au dhalimu kwa kutoitekeleza? Tunaomba ufafanuzi wa hilo.
Jibu: Kuacha kuhukumu kwa Shari´ah ya Allaah kuna aina mbili, kama walivyosema Salaf (Rahimahumu Allaah) kama Ibn ´Abbaas na wengineo:
1 – Ni mtu kuacha kuhukumu kwa Shari´ah kwa kuhalalisha hilo, akaona kuwa hakuna ubaya kuacha Shari´ah, akaona kuwa sheria za kibinadamu ni bora zaidi kuliko Shari´ah, ni sawa nayo au zinajuzu, hata kama Shari´ah ni bora kuliko hizo. Hii aina ni kutoka katika Uislamu na ni ukafiri mkubwa. Ikiwa ataacha Shari´ah huku anaamini kuwa hilo linajuzu na halina ubaya, ni mamoja iwe anapendelea sheria za kibinadamu juu ya Shari´ah au anapendelea Shari´ah, lakini anaona inajuzu kuhukumu kwa nyingine, basi kuamini kuwa inajuzu kuhukumu kwa sheria zisizo za Shari´ah ni ukafiri mkubwa na ufisadi mkubwa.
Watu katika hili wako katika sampuli mbalimbali:
Wapo wanaosema Shari´ah ni bora, lakini si vibaya kuhukumu kwa sheria za kibinadamu.
Wapo wanaosema sheria za kibinadamu ni bora zaidi na zina manufaa zaidi kuliko Shari´ah.
Wapo wanaozifanya sawa, kwa maana wanaona kuwa hakuna tofauti kuhukumu kwa Shari´ah au kwa mawazo ya watu. Haya yote ni kutoka katika Uislamu na ni ukafiri mkubwa.
2 – Ni mtu kuacha kuhukumu kwa Shari´ah kwa sababu fulani na huku anajua kuwa kuhukumu kwa Shari´ah ni wajibu na lazima na ni lazima kwa dola na wengineo kuhukumu kwa Shari´ah, lakini anaacha kwa sababu kama khofu fulani au sababu nyinginezo. Hii ni ukafiri mdogo, dhuluma ndogo na ufuska mdogo. Hivo ndivo walivyosema kikosi cha Salaf kama Ibn ´Abbaas, Mujaahid na wengineo. Katika aina hii ni yale yanayotokea kwa baadhi ya mahakimu wanaohukumu kwa yasiyo ya Shari´ah kwa sababu ya matamanio, rushwa au mfano wa hayo. Haya yote ni katika mlango huu: dhuluma ndogo, ukafiri mdogo na ufuska mdogo. Hili ni kosa kubwa na katika madhambi makubwa, lakini si ukafiri mkubwa, kwa sababu yeye ni mwenye kufanya maasi, anajua kuwa ni mwenye kufanya maasi na kwamba kuhukumu kwa Shari´ah ndiyo wajibu na kwamba haijuzu kuhukumu kwa sheria za watu na kuzipa kipaumbele juu ya Shari´ah. Lakini anaweza kuacha kuhukumu kwa Shari´ah kwa sababu ya matamanio au mambo mengine huku akijua kuwa yeye ni mwenye kufanya maasi. Hivyo amemuasi Allaah na Mtume Wake, ametenda kosa kubwa na katika madhambi makubwa, lakini hilo si katika mlango wa kutoka katika Uislamu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3325/حكم-ترك-تحكيم-شريعة-الله
- Imechapishwa: 03/10/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3325/حكم-ترك-تحكيم-شريعة-الله
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-kuhukumu-kwa-sheria-zilizotungwa-na-wanadamu/