Swali: Sauti haiko wazi….
Jibu: Hili si jambo maalum kwake peke yake. Kumuona Mola katika ndoto kunaweza kumpitia pia mtu mwingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwona Mola wake katika ndoto. Ndoto ni jambo pana. Lakini huenda ikamdhihirikia kitu hali ya kuwa si Mola wake ilihali hajui. Huenda asihukumu kwa yakini kwamba huyo ni Mola wake. Hata hivyo inawezekana mtu kumuona Mola wake katika ndoto kwa namna inayolingana na utukufu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Lakini mara nyingi huwa hajui, kwa sababu hana elimu ya kumtambua kwamba huyo ni Mola wake (Ta´ala). Ama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye anajua. Ndoto za Manabii (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) ni wahy. Tofauti na wengine. Mtu mwingine anaweza kumuona Mola wake, lakini asijue. Huenda akaambiwa: “Mimi ni Mola wako”, lakini asijue kwa sababu ya ukosefu wa elimu na utambuzi. Kwa kuwa kuthibiti kwamba amemuona Mola wake kunahitaji awe amemuona kwa namna ya kumtambua. Kuhusu Manabii wakiona kitu na wakapewa khabari juu yake, basi huo ni wahy kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1810/حكم-روية-الله-عز-وجل-في-المنام
- Imechapishwa: 19/12/2025
Swali: Sauti haiko wazi….
Jibu: Hili si jambo maalum kwake peke yake. Kumuona Mola katika ndoto kunaweza kumpitia pia mtu mwingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwona Mola wake katika ndoto. Ndoto ni jambo pana. Lakini huenda ikamdhihirikia kitu hali ya kuwa si Mola wake ilihali hajui. Huenda asihukumu kwa yakini kwamba huyo ni Mola wake. Hata hivyo inawezekana mtu kumuona Mola wake katika ndoto kwa namna inayolingana na utukufu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Lakini mara nyingi huwa hajui, kwa sababu hana elimu ya kumtambua kwamba huyo ni Mola wake (Ta´ala). Ama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye anajua. Ndoto za Manabii (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) ni wahy. Tofauti na wengine. Mtu mwingine anaweza kumuona Mola wake, lakini asijue. Huenda akaambiwa: “Mimi ni Mola wako”, lakini asijue kwa sababu ya ukosefu wa elimu na utambuzi. Kwa kuwa kuthibiti kwamba amemuona Mola wake kunahitaji awe amemuona kwa namna ya kumtambua. Kuhusu Manabii wakiona kitu na wakapewa khabari juu yake, basi huo ni wahy kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1810/حكم-روية-الله-عز-وجل-في-المنام
Imechapishwa: 19/12/2025
https://firqatunnajia.com/kumuona-allaah-usingizini/