Kumsifu Mtume kwamba ni tiba ya nyoyo na dawa ya afya njema

Swali: Baadhi ya watu wanamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kusema:

اللهم صل على نبينا محمد طب القلوب ودواء العافية

“Ee Allaah! Mswalie Nabii wetu Muhammad, tiba ya nyoyo na dawa ya afya njema.”

Je, hili ni jambo limewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Halikuwekwa katika Shari´ah. Ndani yake kuna utata unaoweza kuleta mkanganyiko kwa watu. Bali swalah bora zaidi juu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni swalah ya Ibraahiym:

اللهم صل على محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد، اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad na jamaa zake Muhammad kama ulivyomsifu Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Hakika Wewe ni Mwenye kusifiwa na Mtukufu. Ee Allaah! Mbariki Muhammad na jamaa wa Muhammad kama ulivyombariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Hakika Wewe ni Mwenye kusifiwa na Mtukufu.”

Swalah hii ndiyo swalah mashuhuri iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imekuja aina mbalimbali. Kwa aina yoyote miongoni mwa zilizothibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisoma mtu, basi amefanya jambo lililosuniwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/309)
  • Imechapishwa: 08/03/2026