Swali: Je, inajuzu kumpa mmoja wa watoto wangu kitu nisichompa mwingine kwa sababu huyo mwingine ni tajiri?
Jibu: Hairuhusiwi kumpa mmoja wa watoto wako wa kiume au wa kike kitu bila kuwapa wengine. Bali ni wajibu kufanya uadilifu baina yao kwa mujibu wa mgawanyo wa mirathi au kuwaacha wote bila kuwapa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mcheni Allaah na mfanye uadilifu baina ya watoto wenu.”[1]
Kuna maafikiano juu yake.
Lakini ikiwa wanaridhia kumpa mmoja wao kitu maalum, basi hakuna ubaya, ikiwa waliokubali ni watu wazima wenye akili timamu. Na pia ikiwa katika watoto wako kuna mwenye udhaifu au asiyeweza kujipatia riziki kwa sababu ya maradhi au hali inayomzuia kufanya kazi na wakati huohuo hana mzazi wala ndugu anayemhudumia, wala hana mshahara wa serikali unaomtosheleza, basi inakulazimu kumhudumia kwa kiasi cha haja yake mpaka Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amtosheleze.
[1] al-Bukhaariy (2587) na Muslim (1623).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/50)
- Imechapishwa: 19/03/2026
Swali: Je, inajuzu kumpa mmoja wa watoto wangu kitu nisichompa mwingine kwa sababu huyo mwingine ni tajiri?
Jibu: Hairuhusiwi kumpa mmoja wa watoto wako wa kiume au wa kike kitu bila kuwapa wengine. Bali ni wajibu kufanya uadilifu baina yao kwa mujibu wa mgawanyo wa mirathi au kuwaacha wote bila kuwapa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mcheni Allaah na mfanye uadilifu baina ya watoto wenu.”[1]
Kuna maafikiano juu yake.
Lakini ikiwa wanaridhia kumpa mmoja wao kitu maalum, basi hakuna ubaya, ikiwa waliokubali ni watu wazima wenye akili timamu. Na pia ikiwa katika watoto wako kuna mwenye udhaifu au asiyeweza kujipatia riziki kwa sababu ya maradhi au hali inayomzuia kufanya kazi na wakati huohuo hana mzazi wala ndugu anayemhudumia, wala hana mshahara wa serikali unaomtosheleza, basi inakulazimu kumhudumia kwa kiasi cha haja yake mpaka Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amtosheleze.
[1] al-Bukhaariy (2587) na Muslim (1623).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/50)
Imechapishwa: 19/03/2026
https://firqatunnajia.com/kumpa-matumizi-mtoto-mmoja-pasina-mwingine/