Swali: Bwana mmoja tajiri ana watoto wengi na ndugu yake ambaye ni fakiri. Je, ni wajibu kwake kumhudumia ndugu yake?

Jibu: Matumizi yanaambatana na urathi. Ikiwa kuna kikwazo kinachozuia kurithi… Mtu huyu hawezi kumrithi ndugu yake, na kwa ajili hiyo sio lazima kumhudumia ndugu yake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ

”Na juu ya mrithi [wa baba kupata] mfano wa hivyo.”

Bi maana matumizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 28/06/2024