Kukodisha duka kwa vinyozi, washonaji au studio za muziki

Swali: Ni ipi hukumu ya kukodisha maduka ya biashara kwa anayefungua duka la kunyoa nywele, kushona nguo za wanawake au kuuza mikanda ya video au mikanda ya nyimbo?

Jibu: Maduka hawakodishiwi kwa wanaoyatumia katika kumuasi Allaah. Bali yakodishwe kwa anayeyatumia katika mambo ya halali. Anayekodisha ili anyoe ndevu za watu, auze vyombo vya upuuzi, auze pombe au kitu chochote cha maasi, haijuzu. Haijuzu katika sehemu yoyote ile, ni mamoja iwe Marekani au kwengine kokote. Ikiwa yeye ni muislamu, basi haijuzu kwake kushirikiana katika maasi ya Allaah, si kwa kukodisha wala kwa namna nyingine yoyote.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30090/حكم-تاجير-المحلات-التجارية-لامور-محرمة
  • Imechapishwa: 07/09/2025