Swali: Je, inafa kukariri Suurah ndani ya Qur-aan kwa wiki mara mbili, mara nne au zaidi?

Jibu: Inafaa kukariri Suurah kwa wiki na kwa siku na hakuna kikomo maalum juu ya hilo. Bali inafaa kuikariri katika Rak´ah mbili tofauti baada ya al-Faatihah katika swalah moja. Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alisoma Suurah katika Rak´ah mbili ya kwanza na ya pili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/81)
  • Imechapishwa: 11/10/2021