Kujizuia kukata nywele, kucha na ngozi Dhul-Hijjah kwa aliyenuia kuchinja

Ukiingia mwezi wa Dhul-Hijjah na yeye amenuia kuchinja basi asikate chochote katika nywele wala kucha zake mpaka achinje. Hili linamuhusu yeye pekee. Kuhusu familia yake hapana vibaya kwao. Linamuhusu yeye pekee aliyejitolea pesa ya kichinjwa. Yeye ndiye asikate chochote katika nywele wala kucha zake mpaka akishachinja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah na akataka mmoja wenu kuchinja, basi asikate kutoka katika nywele wala kucha zake chochote mpaka achinje kwanza.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“… wala chochote katika ngozi yake.”

Kwa maana ya kwamba asikate chochote katika nywele, kucha wala ngozi yake mpaka kwanza achinje. Isipokuwa anayehiji na ambaye anafanya ´Umrah katika yale masiku kumi ya Dhul-Hijjah. Wao hapana vibaya akanyoa katika ´Umrah yake au akapunguza nywele. Vivyo hivyo katika hajj siku ya ´iyd anyoe au apunguze baada ya kurusha vijiwe. Hawa hawakukatazwa, bali wameamrishwa kufanya hivo. Ni lazima wafanye hivo. Makatazo hayawahusu.

[1] Muslim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9190/احكام-الاضحية
  • Imechapishwa: 13/06/2024