Kujifunua mbele ya wavulana wenye uelewa


Swali: Mimi nina ndugu ambaye miaka yake ni kumi na moja na mke wangu anajifunua mbele yake. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Anatakiwa kujisitiri. Kwa sababu huyu amekaribia na pengine hata amekwishabaleghe. Anaweza kuwa anaota au ameshaota nywele za kwapani hata kama ana miaka kumi na moja. Anaweza kubaleghe akiwa na miaka kumi na moja. Kwa ajili hiyo inatakiwa kwa mwanamke – hata kwa yule ambaye amekaribia kubaleghe – ajisitiri mbele yake. Akiwa ni mvulana wa kumi na ameshakuwa na uelewa basi anatakiwa kujisitiri mbele yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/102/%D9%8A%D9%86%D8%A8%D8%BA%D9%8A-%D8%A3%D9%86-%D8%AA%D8%AD%D8%AA%D8%AC%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A3%D8%A9-%D8%B9%D9%85%D9%86-%D9%82%D8%A7%D8%B1%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D9%84%D9%88%D8%BA
  • Imechapishwa: 06/12/2019